Ashukuriwe Mungu Muumba wa mbingu na nchi kwa maana bila yeye nisingekuwa hivi.Hakika yeye ni mkuu na hakuna lisilowezekana kwake.Namshukuru sana kwa uhai,afya,utashi,nguvu na zaidi kwa zawadi ya familia.
Pili,niwashukuru wazazi wangu kwa yote waliyonifanyia tangu nazalia hadi leo,baba kwa kuwa msaada wangu mkubwa na muhimizaji muhimu kuhusu swala zima la shule.Asante ya mama inaweza jaza kurasa na wala hakuna neno linalotosha kubeba ukubwa wa shukrani yangu kwako.Umenizaa,umenitunza,umenilinda na kunipigania. Umefurahi nami kila nilipofurahi,ukawa nami hasa siku nilizokuwa chini na hata pale nilipoanguka na kuonekana si kitu mbele ya walionizunguka ulinishika mkono na kwa ujasiri usio kifani ukaniinua.Ni mengi sana kwa kuyaelezea hila kwa chochote kizuri nilichonacho sasa au km kitakuwa kizuri zaidi baadaye nitazidi kuwashukuru
Tatu ni kwa mdogo wangu wa pekee Neema, ukuu wa Mungu unazidi kujidhihirisha kwangu kwa kunipa wewe kuwa sehemu ya maisha yangu.Hakuna ninalofanya nikitegemea kuwa peke yangu kwa maana najua u pamoja nami kwa kila kitu na kila hali,wewe ni shabiki wangu namba moja na nashukuru sana kwa muda wako wa knisikiliza mambo yangu hata kama mengine huwa ni ya kipuuzi.Asante kwa kusikiliza na kusupport ndoto zangu na kubwa zaidi kwa kuwa mama kwa mwanangu.
Nne kwa marafiki,ndugu zangu na hata majirani zangu.Ahsanteni nyote kwa furaha,maoni na hata changamoto mlizoleta katika maisha yangu.Hakika kila mmoja wenu ana nafasi yake ya kipekee kwangu na nawapenda sana bila kujali mambo yenu na matokeo yake katika maisha yangu.
Mwisho kabisa iwe shukrani ya pekee kwa binti yangu Karen,wewe ni maana halisi ya neno Maisha kwangu.Asante kwa kuwa mvumilivu na muelewa, kutoniona nyumbani kwa kipindi kikubwa katika malezi yako si kitu cha kawaida.Asante kwa kuwa mwanga mpya wa maisha yangu na mpaka mkubwa kwangu dhidi ya ukataji tamaa.Kwa ajili yako ntafanya yooooote ninayotaka na kuhakikisha unapata maisha mazuri.